NEW LIFE IN CHRIST
  • Sign in
  • Register
NEW LIFE IN CHRIST
  • Home
  • About
  • Gallery
  • Contact

Archives

  • February 2025

Categories

  • Uncategorized
  • +255 715 475 837
  • info@newlifeinchrist.or.tz
Twitter Facebook Pinterest Instagram
Home
  • Home
  • About
  • Gallery
  • Contact

About

  1. Home
  2. About

New life in Christ (Maisha mapya ndani ya Kristo)kwa kifupi NLC ni huduma ya wa Kristo walio mpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yao. Yaani wa Kristo waliokoka kutoka madhehebu mbalimbali ya Kikristo

Huduma hii ilianzishwa mwaka 1929 huko Gahini nchini Rwanda. Wakati huo ikijulikana kama East Africa Revival movement. New Life crusade ilitokea ndani ya huduma ya uwamsho wa Afrika Mashariki  uliosambaa kwa kasi ya ajabu katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania

1935 hadi 1962 huduma hii ilienea katika madhehebu mbalimbali inchini Tanzania, ikianzia kutoka kwenye chuo cha ualimu Katoke Mkoani Kagera. Wakati huo faragha zilikuwa chache na ndugu wachache

1963 New Life Crusade ilisajilowa rasmi. Hii ini baada ya Askofu wa Anglican, Askofu Yohana Omari ambaye alitoka kwenye Mkutano wa bill Graham huko mchini uingereza. Huko ndiko kulikotokea jina la New Life Crusade, kwakuwa huduma hiyo ilikuwako huko Uingereza. Katika kipindi chote hicho New Life Crusade ilifanya kazi kubwa ya kuhubiri injili ikijulikana kwa jina hilo. Katika miaka ya 2000 kuliibuka makundi mbalimbali ya uamsho ambayo yalikuwa na majina ya kiharakati. Niwakati huo New Life Crusade ilianza kufikiri kujiondoa kwenye jina la kiharakati, yaani Crusade. Hivyo mwaka 2013 New Life Crusade ikabadili jina na Kujiita New Life in Christ, yaani kwa Kiswahili Maisha mapya ndani ya Kristo. Malengo yake yakibaki kuwa yale yale

Lengo la kuanzishwa kwa New Life in Christ (NLC) ni kuwaleta wa Kristo walio okoka pamoja kutoka madhehebu mbalimbali, Kuwajenga Kiroho wale ambao wameokoka,  Kuhubiri injili ya wokovu kwa watu wote, ili waokoke na kuishi Maisha ya wokovu. Kufanya mikutano ya kiroho ya kuhubiri Injili ya Yeau Kristo, kufanya semina za kiroho kwa ajili ya kuwajenga waKristo ambao wameokoka. Kufanya na kuendesha ibada za faragha (fellowship) kuanzia ngazi ya msingi na eneo kwa lengo la kuwajenga wa Kristo walio okoka ambao wana abudu katika madhehebu mbalimbali

New Life in Christ siyo dhehebu, bali ni huduma inayo unganisha madhehebu mbalimbali ya kikristo, kama ilivyo elezwa hapo awali (Soma Zaidi kiambatanisho cha Ijue New Life in Christ kwenye ukurasa wa tovuti hii

Huduma ya New Life in Christ inaongozwa na Sekretariat katika ngazi ya Taifa. Sekretariat ya Taifa inaundwa na  Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mtunza Hazina na Mtunza hazina Msaidizi. Aidha Katika ngazi ya Taifa kipo chombo kikuu cha maamuzi ambacho kinaitwa Timu ya Taifa, ambayo inaongozwa na Sekretariat ya Taifa, wajumbe wa Sekretariat ya Taifa, wote ni wajumbe wa Timu ya Taifa, wajumbe wengine kwenye timu ya Taifa ni wajumbe wa sekretariat za Mikoa yote ya Tanzania bara na waratibu wa kamati mbalimbali za Taifa

Mfumo huu wa uongozi unasambaa kutoka ngazi ya Taifa hadi ngazi ya Wialya, ambapo kuna viongozi wa mfanano kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu msaidi, Mtunza hazina na Mtunza hazina msaidi

Uwanachama  wa NLC uko wazi kwa mtu yeyote ambaye anamwamini na kumkiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yake,  na anakubaliana na madhumuni ya chama

Makao makuu ya NLC Taifa yako Dodoma. Kuna ofisi za Mikoa katika Mikoa yote ya Tanzania bara na Wilaya zake zote ambazo zina wanachama wa NLC ( Safu ya uongozi itaonyeshwa kwenye ukurasa wa Uongozi)

Tangu kuanzishwa kwake New Life in Christ imefanya kazi nyingi za kuwaleta watu kwa Yesu Kristo, zikiwemo semina, Makongamano, Mikutano mikubwa ya Injili. Kambi za maombi nakadhalika. (kazi nyingi zitaonyeshwa kwenye ukurasa wa matukio na ukurasa wa Picha (Gallery))

Dira (Vision) ya New Life in Crist

Kuwa chama imara cha kuwaleta watu walio okoka na watakao okoka katika umoja wa kikristo wapate kuishi Maisha mapya ndani ya Yesu Kristo siku zote

Dhima (Mission) ya New Life in Christ

Kuwaunganisha watu walio okoka kwa dhumuni la kuwaimarisha kiimani na kuwajengea uwezo wa kutumika katika huduma, ili waweze kushuhudia na kuhubiri Habari njema za wokovu wa Yesu Kristo kwa usahihi, watu wapate kumwamini  na kuokoka

Subscribe to Our Newsletter to Get Daily News!

Sign up now for weekly news and updates

Contact

Call Anytime

+255 715 475 837

Send Email

info@newlifeinchrist.or.tz

Visit Office

Box 1618 Dodoma

Links

  • About Us

Courses

  • Staff login

Featured Posts

February 18, 2025

New life in Christ (Maisha mapya ndani ya Kristo)

© Copyright 2025 New Life in Christ
Twitter Facebook-square Pinterest Instagram

Signin

Lost your password?
Don't have an account Register

Reset Password

Don't have an account Register